RUNALI wafanikiwa kuuza kilo 20.6 milioni za korosho, bei ya juu shilingi 2,610 na bei ya chini shilingi 2,460.
Na Ahmad Mmow.
Chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kilichpo mkoani Lindi kimefanikiwa kuuza tani 20,000 na kilo 600 za korosho ghafi za daraja la kwanza.
Kwenye mnada huo ambao umefanyika leo tarehe 10.11.2025 mjini Nachingwea katika ukumbi wa mikutano wa ofisi kuu ya RUNALI, bei ya juu kwa kila kilo moja ni shilingi 2,610. Ambapo bei ya chinini shilingi 2,460,bei ambazo ziliridhiwa na wakulima waliohudhuria mnada huo.
Akizungumza baada ya wakulima kukubali kuuza kwa bei hizo, mkurugenzi mkuu wa bodi ya korosho Tanzania (Cashewnut Board of Tanzania/CBT), Fransis Alfred aliwaasa wakulima waendelee kulinda ubora wa zao hilo. Kwani bei nzuri zitatokana na ubora.
Alisisitiza wakulima wapeleke korosho maghalani zikiwa zimekauka. Huku wakiepuka kichanya vitu visivyo hitajika.
Huo ni mnada wa kwanza kwa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kwa msimu wa 2025/2026. Lakini ni mnada wa tatu kwa zao hilo kwa msimu wa 2025/2026.
Hadi sasa minada imefanyika katika vyama vikuu vya TANECU(Mtwara), Lindi Mwambao(Lindi) na RUNALI(Nachingwea).

0 Comments