DIWANI AMBUNJE AFURAHIA MAFUNZO YA UTUNZAJI MISITU NA UVUNAJI WA HEWA YA UKAA.

 

Diwani Ambuje afurahia mafunzo ya utunzaji misitu na uvunaji hewa ya ukaa.

Na Ahmad Mmow,  Nachingwea.

Diwani wa kata ya Mpiruka, halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Issa Makota( Ambuje) amewashukuru waandaaji wa mafunzo ya siku mbili kuhusu utunzaji misitu na uvunaji wa hewa ya ukaa. 

Akizungumza kijijijini Mpiruka A, katika halmashauri ya wilaya ya Nachingwea  baada ya kurudi kwenye ziara ya mafunzo ya siku mbili katika halmashauri ya Tanganyika, mkoa wa Katavi. Alisema mafunzo hayo yamemfanya ajue umuhimu na faida za kutunza na kuhifadhi  misitu na kuvuna hewa ya ukaa.

Ambuje ambae aliwashukuru mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Mhandisi Chionda Ali Mfaume Kawawa kwa kukubali kugharamia ziara hiyo na mkuu wa wilaya ya Nachingwea kwa kuibua wazo la mafunzo hayo kwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea alisema ziara hiyo ya mafunzo imekuwa na faida kwa madiwani. Kwani wengi walikuwa hawajui kwamba hewa ya ukaa ambayo inatokana na misitu ni biashara kubwa.

Alibainisha wazi kwamba uharibifu wa misitu licha ya kusababisha mabadiliko ya tabia nchi, lakini pia ni hasara. Kwani kwa kuvuna hewa ukaa vijiji vinaweza kupata fedha nyingi kutoka kwa wahisani.

" Vijiji vya halmashauri ya Tanganyika vimenufaika sana na mradi wa hewa ukaa. Fedha zinazopatikana zinatumika katika sekta za afya, elimu na hata maji. Wananchi wamelipiwa bima ya afya, wanafunzi wa shule wanapata huduma za chakula, nyumba za walimu, vyumba vya madarasa na hata vyoo vya shule zinatumika fedha zinazotokana na mauzo ya hewa ukaa," alisema Ambuje.

Diwani huyo ambae kata yake inaundwa na vijiji vya Mpiruka A na B, Mkumba na Libea amesema vijiji vya halmashauri ya wilaya ya Nachingwea vina nafasi kubwa ya kunufaika na mradi wa hawa ukaa. Kwani vina misitu  ya asili. Kwahiyo kinachotakiwa ni utayari wa wananchi kulinda na kuhifadhi misitu hiyo.

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nachingewa, mkoa wa Lindi walifanya ziara ya mafunzo ya siku mbili katika halmashauri ya wilaya ya Tanganyika. Mafunzo ambayo yalifanyika tarehe 19 na 20.08.2024.



Post a Comment

0 Comments