BODI YA KOROSHO YAWAHIMIZA WAKULIMA WADHIBITI UBORA WA KOROSHO.

 


Bodi ya korosho yawahimiza wakulima wathibiti ubora wa korosho.

Na Ahmad Mmow. 

Wakulima wakorosho nchini wamekumbushwa na kuhimizwa wahakikishe korosho zao zinakuwa na ubora unaostahili kabla ya kupeleka maghalani.

Wito huo kwa wakulima wao hilo umetolewa leo tarehe 09.11.2025 na mkurugenzi mkuu wa bodi ya korosho(Cashewnut Board of Tanzania/CBT), Fransis Alfred alipozungumza na wakulima walihudhuria mnada wa kwanza katika chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao kwa msimu wa 2025/2026.

Bwana Fransis katika mnada huo uliofanyika katika manispaa ya Lindi na kushuhudiwa zikinunuliwa korosho zenye uzito wa tani 5,106 alisema bei za zao hilo zinategemea pia ubora wake katika eneo husika.

Kwakuzingatia ukweli huo, mtendaji mkuu huyo wa CBT aliwahimiza na kuwaasa wakulima wathibiti ubora wa zao hilo kabla ya kupeleka sokoni.

Mtendaji mkuu huyo wa bodi hiyo yenye dhamani ya kusimamia, kuendeleza na kutafuta masoko ya zao hilo alisema wakulima wahekikishe wapeleka korosho zao maghali zikiwa zimekaushwa, hazijachanganywa na vitu ambavyo sio korosho kwa lengo la kuongeza uzito.

Alibainisha kwamba miongoni mwa sababu zinazoweza kuchangia bei ya zao hilo kuwa ndogo ni kukosa ubora. Jambo ambalo pia linasababisha kushindwa kuhimili ushindani sokoni.

" Wanunuzi wanahitaji korosho zenye ubora. Iwapo korosho zinakuwa hazina ubora wanaweza kununua kwa bei ndogo au wasinunue kabisa. Kwani sokoni kuna nchi nyingi zinapeleka zao hili," alisisitiza bwana Fransis.

Kiongozi mtendaji huyo wa bodi ya korosho nchini alisisitiza kwamba korosho zisizo na ubora hazisababishi hasara kwa wakulima wenyewe tu, bali hata kwa taifa. Kwani taswira ya nchi machoni mwa mataifa mengine haiwezi kuwa nzuri.

Amesema kutozingatia ubora kunaweza kusababisha pia wanunuzi wasite kuja kununua korosho za hapa nchini na iwapo watanunua basi ni kwa bei ndogo zisizolingana na gharama uzalishaji.

Post a Comment

0 Comments