KIWANGO CHA UFAULU CHAMKUNA DIWANI, AONESHA FURAHA KWA VITENDO.


 Kiwango cha ufaulu cha mkuna diwani, aonesha furaha kwa vitendo.

Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Kiwango kizuri cha ufaulu na matokeo  ya mtihani wa kidoto cha nne katika shule ya sekondari ya kutwa ya kata ya Mpiruka, halmashauri ya wilaya ya Nachingwea yamemfurahisha na kusababisha diwani wa viti maalum wa halmashauri hiyo, Veronica Makota kutoa zawadi kwa walimu, na wanafunzi waliofaulu vema.

Makota ambae pia ni makamo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi kumi na mbili waliofaulu mtuhani wa kidato cha nne na kuendelea na masomo ya vidato vya tano na sita iliyofanyika jana katika shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Mpiruka A aliwapa wanafunzi hao shilingi 50,000 kila mmoja. 

Diwani huyo ambae anatoka katika kata ya Mpiruka inayoundwa na vijiji vya Mpiruka A, Mkumba, Libea na Mpiruka B, aliwapa pia walimu wa shule hiyo sukari kilo kumi, mchele kilo 20 na mafuta ya kula lita tatu ikiwa ni shukrani kwa  walimu hao kwa matokeo mazuri na kazi kubwa yenye tija waliyofanya.

Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi na fedha hizo ambazo jumla yake ni  takribani shilingi 600,000 alisema  alitoa ili kutimiza ahadi aliyoweka mwaka jana. 

Diwani huyo alibainisha kwamba matokeo na kiwango hicho cha ufaulu hakijawahi kutokea katika shule hiyo  ni mara ya kwanza. Kwahiyo  walimu na wanafunzi waliofaulu hao walistahili pongezi na zawadi.

Aliwaasa wanafunzi waschana waliofaulu na wale ambao bado wanaendelea kusoma katika shule hiyo wasikubali kulaghaiwa na watu wasio watakia mema ambao watasababisha kukatiza ndoto zao kwa kupata mimba.

Lakini pia Makota aliwaonya wanafunzi wavulana wasikubali kuacha masomo na kukimbilia maisha ya mtaani ambayo wakati wowote watayakuta.

"Natamani hali hii iendelelee. Namimi nitawaunga mkono. Sitaraji kusikia mmeacha masomo," Makota alisisitiza.

Akishukuru kwa kupewa zaidi hizo kwa niaba ya walimu na wanafunzi, mwalimu Allan Makwinja licha ya shukrani alimuhakikishia diwani huyo kwamba kasi na kiwango cha ufaulu kitaongezeka. Kwani wamejipanga vema.

Aidha Makwinja aliweka wazi kwamba kitendo kilichofanywa na diwani huyo ni cha kupigiwa mfano. Kwani sio viongozi wengi wanatambua kwa vitendo juhudi za walimu na hata wanafunzi wanaofanya vema katika masomo yao.

Post a Comment

0 Comments