TANECU CHAUZA KOROSHO SAFI GHAFI ZA DARAJA LA KWANZA ZENYE UZITO WA TANI 26,000.

 


TANECU cha uza korosho ghafi za daraja la kwanza zenye uzito wa tani 26,000. 

Na Ahmad Mmow.

Chama kikuu cha ushirika cha TANECU(Tandahimba and Newawala Cooperative Union) leo tarehe 08.11.2025 katika mnada wa kwanza wa zao la korosho hapa nchini kwa msimu wa 2025/2026 kimefanikwa kuuza korosho ghafi za daraja la kwanza zenye uzito wa tani 26,000.



Kwa mujibu wa mmoja wa maofisa wa bodi ya korosho Tanzania(Cashewnut Board of Tanzania/CBT), Amani Ngoleligwe kwenye mnada huo uliofanyika wilayani Tandahimba katika mkoa wa Mtwara bei ya juu ilikuwa ni shilingi 3,520. Ambapo bei ya chini ni shilingi 2,550 kwa kila kilo moja. 

Aidha Ngoleligwe amebainisha kwamba mnada huo ulio hairishwa jana tarehe 07.11.2025 kutokana na changamoto za mtandao umesababisha mabadiliko kidogo ya tarehe za kufanyika minada katika vyama vikuu vingine vya ushirika.

Ameweka wazi kuwa mnada ambao ulitakiwa ufanyike leo tarehe 08.11.2025 katika chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao utafanyika kesho tarehe 09.11.2025. Ambapo mnada wa kwanza kwa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI ambao ungefanyika tarehe 09.11.2020 utafanyika tarehe 10.11.2025 siku ya Jumatatu.

Mnada huo wa korosho uliofanyika leo ni mnada wa kwanza kwa msimu wa mwaka 2025/2026 kwa nchi nzima.

Post a Comment

0 Comments