Lindi Mwambao wafanikiwa kuuza tani 5,106, bei ya juu 2,460 bei ya chini 2,310.
Na Ahmad Mmow.
Chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao kilichopo mkoani Lindi, leo kimefanikiwa kuuza korosho ghafi za daraja la kwanza zenye uzito wa tani 5,106 na kilo 175.
Kwamujibu wa ofisa habari wa bodi ya korosho Tanzania (Cashewnut Board of Tanzania/CBT), Amani Ngoleligwe bei ya juu kwa kila kilo moja imenunuliwa kwa shilingi 2,460. Ambapo bei ya chini ni shilingi 2,310.
Ngoleligwe amebainisha kwamba huo ni mnada wa pili kufanyika katika msimu huu wa 2025/2025. Ambapo mnada wa kwanza ulifanyika jana tarehe 08.11.2025 mkoani Mtwara, wilaya ya Tandahimba katika chama kikuu cha ushirika cha TANECU.
Aidha ofisa huyo wa CBT amesema mnada wa tatu na wakwanza katika chama kikuu cha RUNALI kinachoviunganisha vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) vya wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale utafanyika kesho tarehe 10.11.2025 mjini Nachingwea katika viwanja vya ofisi kuu ya chama hicho.
Mkoa wa Lindi una vyama vikuu viwili vya ushirika ambavyo ni Lindi Mwambao na RUNALI.

0 Comments