Mwenge wa Uhuru kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi ya shilingi 45.9 mkoani Lindi.
Na Ahmad Mmow, Lindi.
Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 utazindua, kuweka mawe ya msingi na kutembelea miradi yenye thamani ya shilingi 45.9 bilioni katika mkoa wa Lindi.
Hayo yameelezwa leo mjini Kilwa Masoko na mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainab Telack baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru na mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohamed Mahamoud.
Mkuu huyo wa mkoa wa Lindi amesema jumla ya miradi 53 iliyopo katika wilaya tano na halmashauri sita zilizopo mkoani humo. Ambapo miradi 13 itazinduliwa, 15 itawekwa mawe ya msingi na 25 itatembelewa.
" Mwenge huu wa Uhuru katika mkoa huu wa Lindi utapita katika wilaya zote tano na halmashauri sita katika kilo meta 1,128," alisema Telack.
Mwenge katika mkoa huo umezindua mradi wa kwanza wa madarasa katika shule ya msingi Kilwa Masoko.
Mwenge huo utakesha katika kijiji cha Kipindimbi. Ambapo kesho utakabidhiwa na kukimbizwa katika wilaya ya Liwale.
0 Comments