SERIKALI WILAYA YA NACHINGWEA YAIPONGEZA BODI YA KOROSHO.

 


Serikali wilaya ya Nachingwea yaipongeza bodi ya korosho.

Na Ahmad Mmow,  Nachingwea.

Bodi ya korosho Tanzania (Cashewnut Board of Tanzania/CBT) kwa usimamizi mzuri wa mauzo ya korosho msimu wa 2025/2026.

Pongezi hizo zimetolewa leo mjini Nachingwea na katibu tawala wa wilaya ya Nachingwea, Haji Mbaruku Balozi alipozungumza na wakulima wakati mnada wa nane na wa mwisho wa zao hilo kwa msimu wa 2025/2026 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI.

Balozi ambae alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Nachingwea kwenye mnada huo alisema bodi ya korosho inastahili kupongezwa  kwa usimamizi mzuri na makini katika kudhibiti ubora na malipo ya wakulima.

Alisema katika msimu wa 2025/2026 malalamiko ya wakulima kuhusu kucheleweshewa malipo ni kidogo ikilinganishwa na misimu mingine.

Aidha katibu tawala huyo wa wilaya ya Nachingwea alisema licha kupungua malalamiko ya wakulima lakini pia hata wanunuzi hawakuwa na malalamiko. Hasa kuhusu ubora wa korosho na ubabaishaji katika kupata korosho walizonunua.

" Furaha ya mkuu wa wilaya yeyote katika mikoa hii ya Lindi na Mtwara nikuona wakulima wanalipwa kwa wakati. Wakulima waliokuja ofini kulalamika msimu huu ni wachache sana na wafanyabiashara wamefurahi na kupongeza pia usimamizi mzuri. Hawausumbuliwa na hawakuiziwa korosho chafu," alisema Balozi.

Katika hali iliyodhihihirisha kwamba hakuwa anatania kuhusu malipo ya wakulima. Aliwaomba wakulima wasio lipwa hadi sasa wapeleke madai yao katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo wakiwa na nyaraka zinazothibitisha bado hawajalipwa.

Lakininpia Balozi aliwaasa wakulima wa korosho wa mikoa ya Lindi na Mtwara wasibweteke. Kwani mikoa mingine imeanza kuja kwa kasi kwa uzalishaji wa zao hilo.

Kwa upande wake nwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, Audax Mpunga licha kuishukuru bodi ya korosho aliwashukuru wakulima kwa kuweza kudhibiti ubora. Ambao umepunguza malalamiko wakati wa malipo. Kwani korosho nyingi ni bora na zilikuwa zinanunulia. Ambapo wakulima walilipwa mapema.

Kwenye mnada huo jumla ya 2,575 ziliuuzwa. Ambapo bei ya juu kwa korosho za daraja la kwanza ilikuwa shilingi 2,410 na bei ya chini shilingi 2 210 kwa kila kilo moja. Ambapo korosho daraja la pili bei ya juu ni shilingi 1,950 na bei ya chini shilingi 1,660 kwa kila kilo moja.

Post a Comment

0 Comments