KAMBONA ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UENYEKITI EA CHADEMA.


 

Kambona atangaza nia ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA.

Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Aliyekuwa katibu wa wa wilaya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa wilaya ya Nachingwea, Geoffrey Kambona ametangaza nia ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Lindi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii jana mjini Nachingwea, Kambona alisema kinachomsukuma kugombea wadhifa huo ni dhamira ya chama hicho kupata   viongozi sahihi wanao weza kuhakikisha  wanaimarisha ujenzi wa chama, madhumuni na malengo ya chama hicho yanafikiwa.

Amesema malengo ya chama hicho ikiwamo katika mkoa wa Lindi ni kuimarisha uwezo wa chama kiuchumi  na viongozi wenye ari ya kufanyakazi za chama, wenye ushawishi, uadilifu na uzalendo kwa chama hicho na nchi kwa jumla.

"Kuwaunganisha wanataaluma mbalimbali waliopo ndani ya mkoa wa Lindi wawe sehemu ya ujenzi wa chama na kuyafikia  makundi yote ya kijamii kwa lengo la kupata jeshi kubwa la kuikomboa Lindi na Kusini kwa jumla," alisema Kambona.

Kada huyo wa CHADEMA akizungumzia wimbi la wanachama wa chama hicho kuhama alisema yeye binafsi hafikirii kwamba kuna siku atakuja kukihama chama hicho. Na kwamba uhenda wanaohama walijiunga na chama hicho bila kujua falsafa na itikadi yake. Kitu ambacho ni tofauti na yeye ambae alijiunga kutokana na kuridhishwa na kufurahishwa na itikadi na falsafa ya chama hicho.

Amesema kwa wapenda demokrasia na maendeleo ya nchi ni vigumu kuhama chama hicho. Kwani ndicho kinasababisha watawala kuwaheshimu wananchi na angalau wanaheshimu na kujali utawala wa sheria.

Kuhusu chama hicho kuwa na nguvu katika wilaya ya Nachingwea kuliko wilaya nyingine za mkoa wa Lindi, Kambona amesema chama hicho chenye madiwani saba katika halmashauri ya wilaya ya Nachingwea ni uimara, uadilifu, uaminifu na jitihada za viongozi waliongoza chama hicho kwa nyakati tofauti hadi sasa katika wilaya hiyo ya Nachingwea. 

Mtia ni huyo alimtaja aliyekuwa mgombea ubunge kupitia chama hicho katika jimbo la Nachingwea mwaka 2020, Dkt Mahadh Mmoto kuwa ni miongoni mwa viongozi na wanachama waliosababisha chama hicho kuwa imara na chenye nguvu katika wilaya ya Nachingwea. 

" Nikichaguliwa na kuwa mwenyekiti. Miongoni mwa mikakati yangu ni kuhakikisha nawatengeneza akina Dkt Mmoto wengi katika mkoa huu ili chama kiwe na nguvu na imara katika mkoa wote wa Linndi," alibainisha Mmoto.

Ratiba ya uchaguzi katika mkoa wa Lindi itatolewa baada ya kuketi kamati kuu kati ya tarehe 3 na 4 mwezi Agosti 2024. Kwahiyo mpaka sasa Kambona hawajui washindani wake kwa nafasi hiyo iwapo atateuliwa na kuwa mgombea.

Post a Comment

0 Comments