TAKUKURU LINDI YASHIRIKISHA WADAU MBALIMBALI KWENYE UCHAGUZI WA SERIAL ZA MITAA.

 TAKUKURU LINDI YASHIRIKISHA WADAU MBALIMBALI KWENYE UCHAGUZI WA SERIAL ZA MITAA.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi yashirikisha wadau mbalimbali kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwa lengo la kuweka mikakati ya kudhibiti rushwa kwenye uchaguzi huo.

Miongoni mwa wadau hao ni pamoja na vyama vya siasa, viongozi wa dini na baraza la wazee, vijana na wanawake, vyombo vya habari pamoja na watu wenye ulemavu.

Akiongea na waandishi wa Habari kwenye kikao cha kutoa taarifa ya utendaji kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2024, Leo Novemba 16,2024 Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi Bi, Asha Kwariko amesema 

“ wadau wa vyombo vya habari vya Mkoa waliazimia kushiriki katika uchaguzi kwa kuzuia na kupambana na rushwa kwa kuwa wanahitaji wapatikane viongozi bora na waadilifu ambao hawajapatikana kwa kutoa rushwa, kwa kuwa nao ndio viongozi waoweza kuimarisha utawala bora na kutokomeza rushwa nchini na wasiwaonee haya wale wote wanao onyesha uhiari na uwezo wa kuhonga au kupokea hongo wakati wa mchakato wa uchaguzi- amesema Kwariko.

Post a Comment

0 Comments