HEART TO HEART YASAIDIA MRADI WA MAJI ZAHANATI YA NAMUPA.
NA HADIJA OMARY
LINDI .....Hatua ya Taasisi ya heart to heart Foundation kwa ufadhiri wa KOICA kuchimba kisima cha maji Katika Zahanati ya namupa iliyopo Katika Kata ya nyangao halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi inaelezwa kuwa ni msaada kwa wanawake wajawazito wanaokwenda kujifungu Katika Zahanati hiyo kutobeba maji kutoka majumbani kwao.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mganga Mfawidi wa Zahanati hiyo Dr. Paul Dominic aliyoisoma mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bi victoria Mwanziva Jana November 15, 2024 wakati wa makabidhiano ya kisima hicho ni kwamba kutokana na tatizo hilo la ukosefu wa maji Katika Zahanati hiyo inawalazimu akina mama wanaofika kwa ajili ya kujifungua kubeba maji kutoka majumbani.
" Katika kipindi ambacho akina mama walikuwa wanakuja kupatiwa huduma ya kujifungua Katika Zahanati yetu walikuwa wanalazimika kubeba maji kutoka majumbani kwao na wengine wanabeba kutoka mtoni kwa ajili ya kuweza kusaidia kukabiliana na upungufu wa maji ulikuwepo na kuweza kukamilisha zoezi mama kujifungua ambalo linahitaji maji mengi".
Hata hivyo Dkt Dominic alisema kuwa kapatikana kwa maji hayo pia kutaweza kusaidia kupunguza magonjwa yote yanayotokana na maji.
Nae Melina Simon Amesema tatizo hilo kilikuwa likiwafanya wamama wajawazito kutoka kijijini wakiwa na maji na pengina yasitosheleze mahitaji na kulazimika kurudi tena nyumbani kwa mara ya pili ili kufuata maji mengine ili kumalizia kupata huduma hiyo.
Mratibu wa Mradi kutoka heart to heart Foundation Innocent Deus Amesema Utekelezaji wa mradi huo ni moja ya kuunga juhudi za serikali katika kuleta maendeleo kwenye jamii husika ambapo kupitia Mradi huo wa miaka mitatu Taasisi hiyo unalenga kufikisha huduma ya maji Safi na salama Katika vituo vya Afya na Zahanati 15 ndani ya halmashauri hiyo ya Mtama.
Amesema Katika kijiji hicho cha Namupa ujenzi huo umehusisha huduma Kwenye Zahanati hiyo pamoja na kusogeza huduma hiyo wananchi .
"Kingine tumeona kulikuwa na changamoto Katika chumba cha kujifungulia ambapo kwenye hicho chumba kulikuwa hakuna huduma ya maji hivyo Katika hii Zahanati ya namupa kwa sababu tumetaka iwe ya mfano tumeunganisha pia huduma hiyo kwenye hicho chumba cha kujifungulia".
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bi victoria Mwanziva akimuwakilisha Mkuu wa mkoa huo mesema kama serikali ya wilaya itaendelea kuthamini mchango unaotolewa na taasisi mbalimbali ikiwemo heart to heart katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kutatua changamoto za wananchi ambapo aliwataka wananchi kulinda miundombinu hiyo ya maji ili idumu kwa muda mrefu.
"Mheshimiwa Rais Samia suluhu Hassan amewekeza Sana Katika sekta mbalimbali, amewekeza Katika sekta ya maji, Elimu, sekta ya Afya lakini tunapowapata Wadau wetu kama hawa heart to heart Foundation wanakuja kuongezea nguvu Sisi hatuna budi Bali ni kuwashukuru Sana Sana"
MWISHOO




0 Comments