ZAIDI YA WANANCHI 100000 KUANDIKISHWA WENYE DAFTARI LA MAKAAZI MANISPAA YA LINDI

 

ZAIDI YA WANANCHI 100000 KUANDIKISHWA WENYE DAFTARI LA MAKAAZI MANISPAA YA LINDI. 



ZAIDI ya Wapiga Kura 100000 wanatarajiwa kuandikishwa kwenye Dafutari la makaazi Katika Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi kufuatia Uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika November 27, 2024. 

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Tellack akizungumza mara baada ya kushiriki zoezi hilo Katika kituo cha uandikishaji cha shule ya msingi Mtanda huko manispaa ya Lindi  amewapongeza wakazi wa mtaa huo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye kujiandikisha kwenye daftari la mkazi.

MKUU wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva akatumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kwenda kujiandikisha kwa wakati ili waweze kuendelea na majukumu mengine na kuepuka msongamano siku za mwisho.

Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Lindi Juma Mnwele Amesema mpaka sasa Hali ya uandikishaji Katika Manispaa hiyo imefika asilimia 17 ambapo matarajio yao kwa siku 10 za uandikishaji wanafikia asilimia 100. 

Nao baadhi ya wananchi walioshiriki zoezi hilo la uandikishaji wamesifu namna ya utaratibu ulivyoweka. 

Aidha zoezi hilo la kujiandikisha kwenye dafutali la makaazi limeanza rasmi tarehe 11 mwezi Oktoba na litaitimishwa tarehe 20 oktoba mwaka 2024. 

Post a Comment

0 Comments