Mpyagila ahaidi neema shule ya sekondari Misufini.

 Mpyagila ahaidi neema shule ya sekondari Misufini.

Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi imejizatiti kuondoa changamoto katika sekta ya elimu katika halmashauri ya wilaya hiyo.

Hayo yameelezwa leo na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Mheshimiwa Adnani Mpyagila(diwani)kwenye mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Misufini ambayo ipo katika kata ya Mpiruka, halmashauri ya wilaya ya Nachingwea.

Mpyagila ambae ni diwani wa kata ya Mbondo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)amesema halmashauri hiyo imejipanga kikamilifu kutatua kero mbali mbali zilizopo katika sekta ya elimu. Kwani katika kuhakikisha azima hiyo inafikiwa imebadilisha matumizi ya fedha za maendeleo kwa kuondoa mfuko huo wa maendeleo kwa kupeleka katika mfuko wa elimu.

" Kulikuwa mfuko wa maendeleo ambao wakulima walikuwa wanakatwa shilingi 30 kwa kila kilo moja. Hata hivyo fedha hizo sasa zitakwenda kutumika katika mfuko wa elimu kwa kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo.

Amesema katika shule hiyo tayari halmashauri ya wilaya hiyo ya Nachingwea imepeleka mbao 200 ambazo zitatumika kwa ujenzi. Huku akiahidi kugharamia kazi zote za kiufundi za ujenzi huo.

Mpyagila aliwahakikishia wananchi waliopo katika halmashauri hiyo kwamba haitawaangusha. Kwani inatambua umuhimu wa elimu.

Post a Comment

0 Comments