Diwani Ambuje.
ahimiza wananchi kujiandikisha, wananchi waahidi kujiandikisha.
Na Ahmad Mmow, Nachingwea.
Wananchi wanaoishi katika kata ya Mpiruka wenye haki na uwezo wa kupiga kura wamehimizwa wakajiandukishe ili watimize haki yao ya kuchagua viongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Wito huo umetolewa leo katika kijiji cha Mpiruka B, kata ya Mpiruka halmashauri ya wilaya ya Nachingwea na diwani wa kata ya Mpiruka, Issa Makota(Ambuje) baada ya kujiandikisha katika kituo cha kujiandikisha.
Akizungumza na wananchi waliokwenda kujiandikisha katika kituo hicho aliwaasa wananchi hao kuwahimiza wenzao wenye sifa za kujiandikisha wajiandikishe.
Amesema kujiandikisha ndiko kutawapa haki ya kupiga kura na kuwachagua viongozi wa vitongoji, mitaa na vijiji ambao wataongoza katika safari ya maendeleo katika maeneo hayo ya utawala.
Ambuje alibainsha kwamba uzoefu unaonesha watu wengi hasa vijana hawapigi kura. Hali ambayo inasababisha wakose haki ya kuongozwa na watu waliowachagua wenyewe.
" Matokeo yake wanaanza kuwalaumu watu waliowachagua viongozi kwamba viongozi waliowachagua hawafai. Wakati nao walitakiwa kuchagua hao ambao wanafaa, tubadilike," alisema Ambuje.
Diwani huyo anaetokana na Chama Cha Mapinduzi alisisitiza kwakusema kila ngazi ya utawala ni kama Ikulu. Na kwamba kwa halmashauri za wilaya ngazi ya utawala kiserikali inaazia kwenye ngazi ya vitingoji. Kwahiyo kuchagua viongozi wa vitongoji, mitaa na vijiji ni muhimu sana. Kwani huko ndiko ngazi ya utawala zinaanzia.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameahidi kushiriki kikamilifu zoezi hilo.
Sofia Almasi mkazi wa Mpiruka A, alisema zoezi hilo ni muhimu na atajiandikisha. Kwani hataki kuchaguliwa viongozi. Bali atachagua mwenyewe bila kujali watatokana na vyama gani. Kwa madai kwamba atachagua viongozi sio chama.
Nae Ramadhan Jamal wa kijiji hicho cha Mpiruka A alitoa wito kwa mamlaka kuzidi kuhamasisha wananchi wajiandikishe. Huku nae akitoa wito kwa vijana wenzake kwenda kujiandikisha. Kwa madai kwamba vijana ndio wanategemewa kuwa viongozi katika ngazi mbalimbali za uongozi.
Bwana Juma Chitanda Ntobho (Somji) wa kijiji cha Mpiruka B alisema nilazima ajiandikishe ili apige kura huku akitoa wito kwa wananchi wenzake wakajiandikishe. Kwani uchaguzi na maendeleo havina chama.
0 Comments