DIWANI AMBUJE AWAASA WAZAZI NA WALEZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU.


 Diwani Ambuje awaasa wazazi na walezi kuwekeza kwenye elimu.

Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Walezi na wazazi waliopo katika kata ya Mpiruka wamekumbushwa kutenga na kutunza fedha kwa ajili ya kugharamia masomo ya watoto wao.

Wito huo umetolewa leo na diwani wa kata ya Mpiruka, Mheshimiwa Issa Makota (Ambije) kwenye mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne waliomaliza katika shule ya sekondari ya Misufini. Mahafali ambayo yalifanyika katika shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Mpiruka A, kata ya Mpiruka halmashauri ya wilaya ya Nachingwea. 

Ambuje amesema suala la elimu kwa mtoto ni lazima. Kwani hakuna urithi mkubwa ambao wazazi na walezi wanatakiwa kuwapa watoto wao ni elimu. Kwahiyo hawana budi kutenga na kuweka fedha kwa ajili ya kugharimia masomo ya watoto wao.

Amesema katika kipindi hiki cha mavuno na mauzo ya korosho wazazi na walezi wanatakiwa wakumbuke kwamba miongoni mwa matumizi muhimu ni kugharamia masomo ya watoto wao.

Alibainisha tabia ya kutotenga fedha kwa ajili ya kugharamia masomo inasababisha changamoto kwa watoto wao wanaofaulu mitihani kushindwa kuripoti shuleni kwa wakati na wengine kushindwa kabisa kuendelea na masomo. Kitendo ambacho ni hasara kwao wazazi na walezi hao. Lakini pia kwa taifa na watoto wao ambao ndoto zao zinakatizwa.

Diwani huyo alisisitiza kwamba licha ya serikali kuandaa mipango na mazingira wezeshi ya kuwafanya watoto wasome bila vikwazo na kutimiza ndoto zao, lakini haiwezi kuwa sababu ya wazazi na walezi kuacha kutimiza wajibu wao wa msingi kwa watoto wao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Mheshimiwa Adnani Mpyagila alisema halmashauri ya wilaya ya Nachingwea imejipanga na kujizatiti kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta ya elimu katika halmshauri hiyo.

Post a Comment

0 Comments