WAKULIMA WAASWA WAKATAE KUTUMIA MIZANI ZA KIZAMANI.

 


Wakulima waaswa wakatae kutumia mizani za kizamani.

Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Wakulima wa ufuta wa mkoani Lindi wameaswa wasikubali kupima ufuta wao kwa kutumia mizani za kizamani badala ya za kisasa(kidigitali) kwenye vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) zenye mizani za kidigitali.

Wito huo umetolewa leo katika kijiji cha Lionja A, kata ya Lionja na ofisa ushirika wa mkoa wa Lindi, Projestus Paschal wakati wa mnada wa kwanza wa ufuta katika chama kikuu cha ushirika cha RUNALI msimu wa 2024.

Paschal ambae alimwakilisha mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika wa mkoa wa Lindi alisema AMCOS zimepata mizani za kidigitali. Kwahiyo  watendaji na viongozi wa AMCOS wanatakiwa kutumia mizani hizo badala ya mizani za kizamani.

Katika kuhakikisha agizo lake kwa viongozi na watendaji wa AMCOS linafanya kazi kikamilifu amewaasa wakulima wakatae kupima ufuta wao kwa kutumia mizani za kizamani katika AMCOS zenye mizani za kidigitali.

Mbali na wito huo mtaalamu huyo wa ushirika aliwataka watendaji kuharakisha uandaaji malipo ya wakulima ili waweze kulipwa mapema.

Alisema wakulima wana mahitaji mengi yanayohitaji fedha. Kwahiyo sio jambo jema kuchelewesha malipo hayo.

Post a Comment

0 Comments