MNADA WA KWANZA WA UFUTA 2024 CHAMA KIKUU CHA RUNALI BEI YA JUU 3,565 BEI YA CHINI 3,350.

 Mnada wa kwanza  wa ufuta 2024 chama kikuu cha RUNALI bei ya juu 3,565, bei ya chini 3,350.

Na Ahmad Mmow,  Nachingwea. 

Mnada wa kwanza wa zao la ufuta katika chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kwa mwaka 2024 uliofanyika leo katika kijiji cha Lionja A, umefanikisha ufuta wenye uzito wa tani 6,896 kununuliwa kwa bei ya juu ya shilingi 3,565 na bei ya chini 3,350.


Katika mnada huo ambao ulifanyika kwa njia ya mtandao kupitia soko la bidhaa(TMX) maghala sita ya RUNALI, EPZA, UMOJA, RUANGWA, EXPORT na Nachingwea DC yalihifadhi ufuta huo.


Akizungumza baada ya kumalizika mnada huo na wakulima kuridhia bei hizo, mwenyekiti wa RUNALI Audax Mpunga aliwaasa wakulima kudhibiti na kutunza ubora wa ufuta ili kuvutia wanunuzi ili wapandishe bei za zao hilo.


Aidha Mpunga aliwataka watendaji wa vyama vya msingi vya ushirika( AMCOS) kuandaa malipo ya wakulima mapema ili walipwe kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments