Waziri Nnauye awataka waandishi waandike habari za chaguzi bila ubaguzi.
Na Ahmad, Dodoma.
Kuelekea uchaguzi mkuu na serikali za mitaa nchini. Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutoa haki kwa wagombea na vyama vyote vya siasa vitakavyo shiriki chaguzi hizo.
Agizo hilo limetolewa jana na leo jijini Dodoma na waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia, Mheshimiwa Nape Nnauye (Mbunge) katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Waziri Nnauye amesema katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa 2024 na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani mwaka 2025, waandishi wq habari hawana budi kuandika habari za wagombea na vyama vyote bila upendeleo na ubaguzi.
Alisema vyama vyote na wagombea wote katika chaguzi hizo wapewe nafasi sawa bila kujali wagombea hao watoka vyama gani, mahali gani, kabila gani na wajinsia gani. Kwani nia ni kuona vyombo vya habari vinatoa haki hiyo kwa usawa.
Waziri huyo mwenye dhamana ya habari, mawasiliano na teknolojia alibainisha kwamba vyama na wagombea wakipewa nafasi sawa ni kuwatendea haki wananchi.Kwani wata wasikia wagombea wote na hata ilani na sera za vyama vyote.
Aliwaasa waandishi kutanguliza uzalendo na masilahi ya nchi katika kuandika habari. Kwani wana wajibu wa kuhimiza amani, utulivu na mshikamano katika taifa hili.
Aidha waziri Nnauye akizungumzia Uhuru wa vyombo vya habari nchini alisema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya utendaji kazi na uhuru wa vyombo vya habari. Na tayari kumekuwa na Uhuru huo, kwani fungia fungia ya vyombo vya habari imepungua kama siyo kwisha kabisa.
Amesema ingawa bado zipo changamoto chache lakini hali ya sasa hailingani na hali ya miaka ya nyuma. Nakwamba juhudi zinaendelea.
Amebainisha kwamba baadhi ya sheria zimerekebishwa na nyingine zitarekebishwa baada ya kuzifanyia marekebisho ya sera. Kwani changamoto ni kwamba sheria ili iweze kurekebishwa ni lazima sera zinazohusiana na sheria husika zirekebishwe.
Hiyo ni mara ya pili waziri Nnauye kueleza hayo. Kwani jana wakati anazindua maadhimisho hayo alieleza. Ambapo leo wakati ana mkaribisha waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa(Mbunge) alirudia tena.

0 Comments