WANAHABARI WAASWA KUANDIKA KWA KINA HABARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI.



 Wanahabari waaswa kuandika kwa kina habari za na mabiliko ya tabia nchi.


Na Ahmad Mmow, Dodoma.


Waandishi wa habari nchini wameaswa waandike habari zinazohusu mazingira na tabia nchi.


Wito huo umetolewa leo jijini Dodoma na waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kwenye hotuba yake katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.


Waziri mkuu amesema waandishi wa habari wanawajibu wa kuhamasisha wananchi mambo yanayohusu mazingira na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Kwahiyo wanatakiwa kuandika habari za mazingira na athari za mabadiliko hayo ya tabia nchi kwa kina.


Amebainisha kwamba habari za mazingira licha ya kuwa na umuhimu mkubwa lakini changamoto iliyopo ni idadi ndogo ya waandishi wanaoandika habari za mazingira kwa kina.


Amewaasa waandishi wawakumbushe na kuwahamasisha wananchi wajibu wao wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Huku akiongeza kuwakumbusha kwamba wanachi wengi hawajui athari za tabia nchi. Kwahiyo ili waweze kutimiza wajibu huo ni vema waandishi wawape elimu inayohusu mazingira.


Waziri mkuu ameongeza kusema kwamba wanahabari wanawajibu huo wa kuiunga mkono serikali katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira. Kwani asilimia 50 ya wananchi wanatumia kuni. Huku asilimia 20 inatumia mkaa. Hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira kutokana na kukata misitu.


Waziri mkuu huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewahakikishia waandishi wa habari nchini kwamba serikali itaendelea kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa uhuru bila kubughuziwa na kuingiliwa.


Katika hali inayothibitisha kwamba serikali inatambua, kuheshimu na kutambua umuhimu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari hapa nchini watendaji wanaoratibu ziara za viongozi wakiwamo makatibu tawala wa mikoa kuandaa usafiri maalum na uhakika wa waandishi wa habari wanakuwepo kwenye ziara za viongozi hao. 


Huku akiweka wazi kwamba waandishi hawatakiwi kupata matatizo wala hofu wanapokuwa kwenye ziara hizo na hata nje ya ziara wanapotimiza majukumu yao. Na kwamba kuwapa usafiri maalumu na wa uhakika kutarahisisha kuandaa habari na kutuma haraka kwenye vyombo wanavyofanyia 

kazi.

Post a Comment

0 Comments