WAZALISHAJI CHUMVI LINDI WAIOMBA SERIKALI IWAPIGE JEKI NA IREKEBISHE BARABARA.

 


Wazalishaji chumvi Lindi waiomba serikali iwapige jeki na irekebishe barabara.

Na Ahmad Mmow.

Kufuatia kuharibika mashamba ya chumvi kutokana na mvua zilizo sababishwa na kimbunga hidaya. Wazalishaji chumvi katika wilaya ya Lindi wameomba serikali iwawezeshe fedha kama ruzuku ili waweze kurekebisha mashamba hayo.

Leo wakizungumza mjini Lindi. Wazalishaji chumvi hao wamesema mashamba mengi yameharibiwa na mvua. Hali ambayo itasababisha kushindwa kuzalisha chumvi na wananchi takribani 4,500 kukosa ajira.

Afwilile Mbembela, ambae ni mwenyekiti wa mkoa wa kitengo cha uzalishaji chumvi mkoa qa Lindi(LIREMA) alisema wilaya ya Lindi pekee ina mashamba 177. Ambapo mkoa wa Lindi una mashamba takribani 293. Hatahivyo takribani robo tatu ya mashamba hayo yameharibiwa na mvua. Hali ambayo itasababisha wananchi takribani 4,500 kuwa kwenye hatari ya kukosa ajira. Kwani wananchi hao ambao wengi ni wanawake walikuwa vibarua kwenye mashamba hayo.

" Kutokana na hali hii tunaomba serikali itupatie fedha kama ruzuku ambayo itatumika kurekebisha mashamba hayo. Vinginevyo hali itakuwa ngumu kwetu wazalishaji na hata wananchi hao ambao walikuwa wanafanya kazi kwenye mashamba hayo.

Nae Rafiki Ghazal ambae ni katibu wa LIREMA alisema lichaha ya kupewa ruzuku serikali ifanyie matengenezo barabara zinazokwenda katika mashamba hayo. Kwani kutokana na uharibifu uliosababishwa na mvua hizo hayafikiki.

" Tunatambua kwamba serikali mwaka huu ina kazi kubwa ya kurejesha miundombinu ya barabara katika maeneo mengi hapa nchini, lakini tuomba barabara hizo zifanyiwe matengenezo," alisema Ghazal.

Ghazal aliyataja baadhi ya maeneo ambayo yana mashamba lakini hayafikiki kuwa ni Matope, Mkwaya, Kinyenyei, Mingoyo, Liteta, Kwa Adam Ali, Kiduni, Ngurumahamba, Mtange na Mchinga.

Kwa upande wake mzalishaji chumvi Mohamed Chimbuli alisema kunahaja ya serikali kuwapa fedha kama ruzuku ili uzalishaji uendelee. Kwani bila ya kuzalisha na kuuza watashindwa kulipa tozo ambazo wanadaiwa na mamlaka ya mapato( TRA) na halmashauri ya manispaa ya Lindi. Maelezo ambayo yaliungwa mkono na mzalishaji mwingine, George Gwaje.

Mkoa wa Lindi ni miongoni mwa mikoa iliyoathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua zilizosababishwa na kimbunga Hidaya hapa nchini. Hali ambayo imesababisha barabara nyingi ikiwamo barabara ya Dar-es-Salaam-Mtwara kuharibika.

Post a Comment

0 Comments