Wana CCM Nachingwea washauriwa kuunga mkono juhudi za mwenyekiti kujenga chama imara.
Na Ahmad Mmow, Nachingwea.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani Nachingwea wameaswa kuunga mkono juhudi za mwenyekiti wa taifa wa chama hicho ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan katika kujenga chama imara kinachojitegemea.
Wito huo kwa wanachama wa CCM wa wilaya ya Nachingwea umetolewa leo mjini Nachingwea na kada wa chama hicho, Mohamed Ungele baada ya kukabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi 500,000 ambavyo vitatumika kwa ujenzi wa nyumba ya kuishi katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM(UWT) wilaya ya Nachingwea.
Ungele ambae alikabidhi mifuko kumi ya saruji na nondo kumi alisema wanachama wa CCM hawana budi kuunga mkono jitihada za mwenyekiti wa taifa wa chama chao ambae anataka kiwe na uchumi imara na kinachojitegemea.
Alibainisha kwamba miongoni mwa kuunga mkono juhudi hizo ni kutoa michango katika shughuli na kazi za maendeleo ya chama. Ikiwamo ujenzi wa ofisi za chama, jumuia na nyumba za watumishi.
Kwa upande wake katibu wa wilaya wa jumuia hiyo, Halima Tina licha ya kumshukuru kwa m
kada huyo alitoa wito kwa wanachama wa chama hicho na jumuia zake kuchangia miradi mbali mbali inayoanzishwa na kutekelezwa na chama hicho.
0 Comments