Spika Dr Tulia atoa wito kwa taasisi za serikali.
Na Ahmad Mmow, Dodoma.
Taasisi za serikali zinazodaiwa na vyombo vya habari vimeombwa kulipa madeni hayo.
Wito huo umetolewa leo mjini Dodoma na spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Tulia Akson alipokuwa anazindua maadhimisho ya 31 ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani. Ambayo kitaifa yanafanyika jijini Dodoma.
Dr Tulia alisema miongoni mwa changamoto zinazovikabili vyombo vya habari ni uwezo mdogo wa kiuchumi.
Alisema kutokuwa na uwezo wa kiuchumi ambao ungesababisha vyombo hivyo kuwa imara kumechangia baadhi ya vyombo kufungwa baada ya kushindwa kujiendesha.
Kwakuzingatia ukweli huo kiongozi mkuu huyo wa Bunge la Jahmri ya Muungano wa Tanzania ametoa wito kwa taasisi za serikali zinazodaiwa na vyombo vya habari zilipe ili viweze kugharamia uendeshaji wake.
Alibainisha kwamba Uhuru wa vyombo vya habari hauwezi kukamilika iwapo vyombo vya habari havitakuwa imara na madhubuti kiuchumi.
Mbali na wito huo kwa taasisi za serikali zinazodaiwa na vyombo vya habari Dr Tulia alitoa wito kwa waandishi wa habari nchini kusaidia kuhamasisha wananchi kuhusu utunzaji wa mazingira na athari hasi za mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema serikali ina imani na inavitegemea vyombo vya habari katika kuhamasisha wananchi utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi. Kwani wananchi wengi hawajui kuwepo mabadiliko ya tabia nchi na matokeo ya mabadiliko hayo.
" Takribani watu milioni kumi na sita wanaoishi katika maeneo ya Pwani wanategemea mazao ya bahari kuendesha maisha yao hata hivyo kuna uchafuzi wa mazingira. Ikiwamo utupaji taka ngumu kama mifuko ya plastiki," alisisitiza Dr Tulia.
Kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa kesho kwa ngazi ya taifa.
0 Comments