Nahukahuka waishukuru serikali .
Na Ahmad Mmow, Mtama.
Kufatia kukamilika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nahukahuka,halmashauri ya Mtama, wilaya ya Lindi. Wananchi wa kkijiji hicho wameishukuru serikali kwa ujenzi wa zahanati hiyo.
Wamesema kukamilika kwa huo ujenzi na kuanza kutumika kwa zahanati hiyo kumewaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya. Ikiwamo matibabu.
Wananchi hao walieleza hayo leo kijijini hapo baada ya uzinduzi wa zahanati hiyo uliofanywa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Godfrey Mzava.
Wakizungumza kwaniaba ya wananchi wenzao, mabibi
Brigita Bernad na Paulina Lukas walisema walikuwa wanatembea umbali wa takribani kilometa tano ili kufika katika kijiji cha Nyangamamara kupata matibabu na huduma nyingine za afaya. Hali ambayo ilisababisha baadhi ya akina mama wajawazito kujifungulia njiani. Huku wengine wakipoteza maisha kabla ya kufikishwa Nyangamara.
Nae kaimu ofisa mtendaji kata, Hamisi Chande alisema ujenzi wa zahanati hiyo hadi kukamilika umegharimu shilingi 68,500,000 ambazo zinajumuisha michango ya wananchi.
"Ndugu kiongozi wa mbio za za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 ujenzi wa zahanati hii umetumia gharama ya ujenzi wa zahanati hii umetumia nguvu za wananchi, halmashari ya Mtama, mfuko wa jimbo na serikali kuu," alisema Chande.
Mwenge wa Uhuru leo upo katika halmashauri ya Mtama ikiwa ni halmashauri ya nne kati ya sita zilizopo katika mkoa wa Lindi ambazo tayari umekimbizwa. Ambapo halmashauri hii ya Mtama ilikabidhiwa leo kutoka kwa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea.
Kesho halmashauri ya Mtama kwa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa ambayo itakuwa halmashauri ya tano kati ya hizo sita zilizokimbizwa na kutembelewa na Mwenge huo wa Uhuru.
0 Comments