Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ahimiza kutunza miradi ya maendeleo.
Na Ahmad Mmow, Nachingwea.
Wananchi na watumishi wa umma wametakiwa kutunza na kulinda miradi ya maendeleo na miundombinu inayotekelezwa na iliyopo katika maeneo yao.
Agizo hilo limetolewa leo na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Godfrey Mzava katika kijiji cha Nditi, wilaya ya Nachingwea, mkoa wa Lindi. Baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa madarasa matano na ofisi ya walimu katika shule ya msingi ya Nditi.
Amesema kuna haja ya kutunza na kulinda miradi na miundombinu inayotekelezwa na iliyopo katika maeneo yao. Kwani miradi hiyo imetumia fedha nyingi . Kwahiyo kutunza na kulinda kutasababisha miradi na miundo mbinu hiyo kutumika kwa muda mrefu.
Mzava pia amewataka walimu na wananchi wa kijijihicho kutunza majengo hayo ili yaweze kutumika kwa muda mrefu na kuwezesha wanafunzi wapate elimu kwenye mazingira mazuri na bora.
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa alibainisha kwamba majengo mengi yanayojengwa kwa ubora yana haribika haraka kwa kukosa matunzo na kulazimika serikali kutenga fedha za ukarabati ambazo zingeweza kutumika kwenye miradi mingine.
Aidha Mzava ameipongeza serikali ya kijiji hicho kwa ujenzi huo ambao umetumia shilingi milioni 153. Fedha ambazo zimetokana na tozo ya ushuru wa mgodi wa madini ambao upo katika kijiji hicho.
Mwenge wa Uhuru leo upo katika wilaya ya Nachingwea. Ambapo kesho tarehe 27.05.2024 utakabidhiwa na kupokewa katika halmashauri ya Mtama.
0 Comments