NENO LA SHUKRANI KUTOKA KWA MWENYEKITI.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Lindi, Fatuma Maumba, anapenda kutumia fursa hii kutoa shukrani za dhati
kwa upendo, faraja, na msaada mkubwa ambao tumeupokea kutoka kwenu na wengine
wote ambao mmetusaidia katika wakati huu mgumu wa kuwapoteza wapendwa wetu,
Abdallah Nanda (Channel ten) na Josephine Kibiriti (Star Tv) ambao walikuwa
wawakilishi mkoa wa Lindi.
Naomba nitoe shukrani za pekee kwa wale ambao walitoa
mchango wao wa kifedha na kumkabidhi Mwenyekiti kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Lindi, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, CCM mkoa wa Lindi, Mama Salma Kikwete, Bodi ya
korosho, Chama cha ushirika Lindi Mwambao, Bandari ya Mtwara (PTA), Ofisi ya
Mganga Mkuu mkoa wa Lindi na wadau wote waliotoa mmoja mmoja. Upendo wenu
umetupa nguvu na kutufanya tujisikie wenye bahati kuwa na marafiki kama nyinyi.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika
maisha yenu na awape amani tele. Tuna imani kwamba wapendwa wetu sasa wapo mahali
pema na amani ya milele.
Tena, shukrani nyingi kwa wote ambao wamekuwa pamoja nasi
wakati huu wa majonzi. Mwenyezi Mungu awabariki nyote.
Kwa upendo na shukrani tele,
![]()
Fatuma Maumba
Mwenyekiti
Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Lindi (LRPC).

0 Comments