VIKUNDI 111 LINDI VYAPEWA MIKOPO YA ASILIMIA 10%.
Na Said Hamdani, LINDI.
Februari 06:JUMLA ya Sh,450,000,000/-zimeidhinishwa na kutolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,ikiwa ni Mikopo ya Asilimia 10% iliyoidhinishwa na Serikali kwa vikundi mbalimbali vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu waweze kujikwamua kiuchumi.
Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Dr Danford Mwakatege katika hafla ya uzinduzi utoaji Mikopo ya robo ya pili kwa vikundi (111) iliyofanyika uwanja wa Ilulu mjini hapa.
Alisema kutolewa kwa mikopo hiyo inatokana na Serikali kuruhusu baada ya kuzuiliwa kufanya tathimini na kufunguliwa tena,kisha makundi kusajiliwa kupitia mfumo maalumu ikiwemo kamati za usimamizi za huduma za mikopo ngazi za kata,Halmashauri na Wilaya.
Dr Mwakatege ametaja makundi 538 yatakayonufaika na Mkopo huo, wapo wanawake 367 na wanaume 147,vilivyobaki vitapewa kufuatia urejeshaji kupitia vikundi (111) vilivyopatiwa awamu hii ya robo ya pili.
“Awamu hii robo ya pili vikundi vikavyopewa Mkopo wa Leo hii ni (111) na vilivyoki vitakabidhiwa awamu nyingine kutegemea na urejeshaji utakavyokwenda kwa waliokopeshwa”Alisema Dr Mwakatege..
Alisema mikopo imetolewa kwa vikundi hivyo (111) kati ya 544 vilivyojitokeza kuomba na kukamilisha maandiko na taratibu zingine kupitia kamati husika.
Kaimu mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Lindi alifafanua kwa kueleza kwamba Sh,216,311,000/-zimetolewa kwa vikundi (58) vya wanawake, Sh,180,000,000/-vimepatiwa vikundi (34) vya vijana na Sh, 53,689,000/-zimekwenda kwa vikundi (19) vya watu walio na ulemavu.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwamviva aliyekuwa mgeni rasmi kuzindua utoaji wa Mikopo hiyo,amevipongeza vikundi hivyo na kuvisisitiza kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini unaowakabili kila uchwao.
Aidha,amewasisisitiza kurejesha Mikopo waliochukuwa kwa wakati uliopangwa waweze kukopeshwa na makundi mingine yaliyobakia.
‘Ndugu zangu,wazee wangu kama Mikopo hii mliyopewa mkaitumie kwa makusudio ya kujikwamua kiuchumi na sio mahali ya kwenda kufunga ndoa”Alisisitiza Mwamviva.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa mikopo hiyo,Somoe Juma,Hadija Athumani, Hemedi Daudi na Isumaili Haji wamehaidi kuitumia kwa malengo waliyoyapanga na si vinginevyo,ikiwemo kufanyia ufuska.
Pia wamehaidi kurejesha kwa wakati uliopangwa ili na wengine waweze kukopeshwa na wao kuendelea kukopa tena kwa lengo la kuongeza mitaji yao kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
MWISHO.
0 Comments