WAZAZI NA WALEZI WAAZIMIA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI CHIMINULA.


 Wazazi na walezi waazimia kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati shule ya msingi Chiminula.

Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Chiminula, halmashauri ya wilaya ya Nachingwea katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati wamekubaliana kugharamia matengenezo ya madawati 26 yenye thamani ya shilingi 2,600,000.

Wazazi na walezi hao walikubaliana na kufanya uamuzi huo jana katika mkutano wa wazazi na walezi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo. Mkutano ambao ulifanyika shuleni hapo.

 Waliazimia kwamba yatengenezwe na kuanza kutumika mwezi Januari 2025. Mwezi ambao shule zitafunguliwa na kuanza muhula mpya. Ambapo kila mzazi atachangia shilingi 12,000.

Mbali na madawati walikubaliana kuchangia shilingi 10,000 kila mmoja zitakazotumika kwa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa. Mchango ambao pia unawahusu wananchi wote wa kijiji cha Mpiruka A. Kijiji ambacho kina miliki shule hiyo.

Katika hatua nyingine wazazi hao walitoa wito kwa wazazi wenzao ambao hawajalipa mchango wa mpishi wa chakula cha wanafunzi walipe haraka kabla muhula mpya kuanza. 

Awali mwalimu kiongozi(mwalimu mkuu), Mwalimu Maskati aliwaeleza wazazi na walezi hao kwamba shule hiyo ambayo mwaka 2025 itaanza kuwa na wanafunzi wa darasa la tano haina madawati ya kutosha. Huku akiweka wazi kwamba yanahitaji madawati 26 ambayo thamani yake ni shilingi 2,600,000.

Shule ya msingi Chiminula iliyopo katika kijiji cha Mpiruka A, kata ya Mpiruka, halmashauri na wilaya ya Nachichingwea mkoa wa Lindi inajumla ya wanafunzi 220.

Post a Comment

0 Comments