KATIBU WA MBUNGE UNGELE ATOA RAI KWA WAKULIMA WA KOROSHO.

 


Katibu wa mbunge Ungele atoa rai kwa wakulima wa korosho.

Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Katika kuhakikisha bei za korosho haziendelei kushuka katika mkoa wa Lindi msimu huu wa 2024/2025 wakulima wameaswa waendelee kuthibiti ubora wa zao hilo.

Wito huo umetolewa hivi karibuni mjini Nachingwea, na Fatuma Umbili ambae ni katibu wa mbunge wa viti maalumu wa mkoa wa Lindi(CCM) Theclar Ungele kwenye mnada wa korosho wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chama hicho.

Umbili alisema kushuka kwa bei za korosho katika minada ya sasa ambayo inaelekea mwishoni kunachangiwa na korosho kukosa ubora. Hasa kutokana na mvua ambazo zimeanza kunyesha katika baadhi ya maeneo katika mkoa huu wa Lindi.

Kwakuzingatia ukweli huo, Umbili alisema ili bei zisiendelee kushuka nilazima wakulima wathibiti ubora wa korosho kwa kuanza kuzianika juani walau kwa muda wa siku mbili kabla ya kupeleka maghalani.

Alibainisha kwamba kutothibiti ubora wa zao hilo kutachangia bei za zao hilo kuendelea kushuka na kukosa wanunuzi. Kwani tayari katika mnada huo baadhi korosho zilikosa wanunuzi.

Aidha katibu huyo wa mbunge aliishukukuru serikali kwa kuanzisha mfumo wa ununuzi wa mazao kwa njia ya Soko la Bidhaa Tanzania(TMX). Kwani umeondoa malalamiko kutokana na uwazi unaofanyika kwenye minada.

Katika mnada huo wa tisa kwa chama kikuu hicho cha ushirika cha RUNALI bei ya korosho za daraja la kwanza ilikuwa shilingi 2,510. Huku bei ya chini ikiwa ni shilingi 2,310 kwa kila kilo moja. Ambapo tani 2,500 za korosho za daraja hilo la kwanza zimenunuliwa.

Post a Comment

0 Comments