RUNALI CHAUZA TANI 1880. 753 ZA KOROSHO, CHATARAJIA KUFANYA MNADA MWINGINE.


RUNALI CHAUZA TANI 1880. 753 ZA KOROSHO, CHATARAJIA KUFANYA MNADA MWINGINE.

Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kilichopo mkoani Lindi kupitia mnada wake wa 11 kwa msimu wa 2024/2025 uliofanyika leo mjini Nachingwea kimefanikiwa kuuza korosho ghafi zenye uzito wa tani 1880 na kilo 753.

Katika mnada huo uliokuwa na mafungu 14(loti) za korosho za daraja la kwanza na lapili, korosho za daraja la kwanza zimeuzwa kwa bei ya juu ya shilingi 2,160 na bei ya chini shilingi 2010 kwa kila kilo moja.

Aidha korosho za daraja la pili zenye uzito wa tani 892 na kilo 316 ziliuzwa kwa bei ya juu ya shilingi 1,710. Ambapo bei ya chini ni shilingi 1,650 kwa kila kilo moja.

Mbali na hayo, chama hicho licha katika mnada wa kumi kutangaza kwamba mnada huu wa kumi na moja uliofanyika leo ungekuwa wa mwisho kwa msimu huu, lakini bado kinatarajia kufanya mnada mwingine.

Mwenyekiti wa chama hicho, Audax Mpunga amesema kutokana na changamoto ya uhaba wa vifungashio bado kuna korosho katika baadhi ya maghala ya vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) ambavyo vipo chini ya RUNALI. 

" Tulitarajia mnada huu ungekuwa wa mwisho. Hatahivyo bado kuna maghala yenye korosho tunalazimika kufanya mnada mwingine ili korosho zote ziweze kuuzwa," alisema Mpunga.

Lakini pia mwenyekiti huyo alisema kutokana na baadhi ya vyama vikuu kufunga msimu wa ununuzi wa zao hilo baadhi ya wakulima waliopo kwenye vyama hivyo wanaleta korosho zao katika AMCOS zilizo chini ya RUNALI. Hali ambayo inasababisha kuwepo umuhimu wa kufanya mnada mwingine.

Post a Comment

0 Comments