MNADA WA NNE WA KOROSHO LINDI MWAMBAO, BEI YA JUU SH. 3,340 NA CHINI SH. 3,040.

MNADA WA NNE WA KOROSHO LINDI MWAMBAO, BEI YA JUU SH. 3,340 NA CHINI SH. 3,040

KIASI cha tani 6502 na kilo 73 za korosho ghafi zimeuzwa kwa bei ya juu Sh.3340 na bei  ya chini, Sh. 3040 katika mnada wa nne wa zao hilo uliofanywa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwambao.

Mnada huo umefanyika Novemba 2, 2024 kupitia mfumo wa TMX katika Chama cha Msingi cha Ushirika Mnolela.

Aidha Nurudini Swala meneja wa Chama kikuu Cha ushirika Lindi mwambao amesema minada yote iliyopita pamoja na na waleo yote imeenda sawa na zaidi ya tani Elf sita zimeuzwa Leo.

Swala Amesema malipo ya minada yote inaendelea kulipwa na  zaidi ya Shilingi billioni hamsini nane nane zimelipwa.

"Niwaombe wakulima waendelee kukusanya Korosho zao kwa wakati kwasababu Hali ya hewa imeanza kubadilika na mvua zimesha anza kunyesha"amesema Swala 

Mohamed ISSA mkulima wa Korosho Amesema baada ya kusikia Bei hiyo ameishukuru kuona Bei ya Leo imeongezeka baada ya mnada wa pili kushuka Bei  wamerudi na tumaini jipya.

"Tunaishukuru sana serikali na vyama vyetu vya ushirika kuendelea kutusimamia katika uuzaji huu wa Korosho wanamnolela tumeridi na tumaini jipya"Amesema Mohamed. 

Athumani Muidini mkazi wa Mnolela Amesema kwa mnada wa Leo amejiridhisha kuona mnada umefanyika kwenye amkosi yao na kushuhudia Korosho zao zikiuzwa.

"Tunamshukuru mungu Allamdulilah kwa Bei hii ya Elf 3340 na matarajio yetu minada yote itaenda sawia kwa minada yote iliyopita na itakayo endelea itaenda vizuri.

Post a Comment

0 Comments