Katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Leo November 25 kumefanyika maandamano ya amani ya kupinga ukatili katika Mkoa wa Manyara.
Maandamano hayo yamafanyika Asubuhi ya leo ambayo yameanzia katika viwanja vya stendi ya zamani iliyoko katika mji wa Babati Hadi katika ukumbi wa white rose ambapo waandamanaji wametembea kwa zaidi ya km 10.
Maandamano hayo yameandaliwa yamewashikisha makundi mabalimbali wakiwemo wafanyabiashara wa Mkoa wa Manyara, Waandishi wa Habari, wanavyuo, maaafisa usafirishaji na wadau mbalimbali.
Aidha, maandamano hayo yameandaliwa na umoja wa club za waandishi wa habari Tanzania (UTPC), club ya waandishi wa habari Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kwa lengo la kusambaza ujumbe katika jamii wa kupinga vitendo vya ukatili.
#EndGBV #16DaysOfActivism #EmpowerWomenAndGirls #GenderEquality #Media #WomenJournalists
@kennethsimbaya
@swedenintz
@tamwa_
@womenfund_tz
@manyara_press_club
@wizarahmth
@gwajimad
@watotowetutunuyetu


0 Comments