KIJANA JELA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUBAKA MSICHANA MDOGO.

 


KIJANA JELA MIAKA 30 Kosa LA KUBAKA MSICHANA MDOGO.

Na Said  Hamdani, LINDI.

Novemba 04/2024:MKAZI Kata ya Ng’apa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,Shakiri Selemani Kazembe (24) kutumikia kifungo cha miaka 30 Gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kumkabaka msichana mwenye umri wa 15 jina limehifadhiwa.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahaka ya Wilaya ya Lindi,Dethimini Kimathi baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.

Kabla kutolewa kwa hukumu hiyo, Hakimi Kimathi alimuuliza mshitakiwa kama analo neno litaloishawishi Mahakama isimpe adhabu kali, akaomba asipewe adhabu kali kwa ni mkosaji wa mara ya kwanza anayo familia wazazi wawili wanamtegemea.

“Mheshimiwa Hakimu naomba usinipe adhabu kali kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza pia nina familia wazazi wawili wananitegemea huduma yangu” Alijitetea Rajabu..

Baada ya utetezi huo, Hakimu Kimathi alimuuliza mwana sheria wa Serikali Hilali Hamza kama ana kumbukumbu makosa ya zamani kwa mshitakiwa na kujibu hana,huku akiomba apewe adhabu kali iwe fundisho kwake na wengine walio na tabia hiyo.

“Mheshimiwa, sina kumbukumbu zake makosa ya zamani kwa mshitakiwa,lakini naiomba mahakama yako tukufu impe mshitakiwa huyu adhabu kali”Alisema Hamza.

Hamza alidai kwamba kitendo kilichofanywa na mshitakiwa kumbaka msichana mwenye umri mdogo ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza ni unyama usiostamilika kwa jamii.

Hakimu Kimathi akitoa hukumu katika kesi hiyo Namba 6586/2024 kupitia vifungu 130 (1) 2 (e) na 131 (1) Sheria sura ya adhabu 2022 amesikiliza maombi ya pande zote mbili,lakini Sheria inamshika mikono na kumuhukumu Kazembe kutumikia kifungo cha miaka 30 Gerezani.

Awali ilidaiwa na mwanasheria wa Serikali Hamza kwamba Machi 10/2024,Kijiji cha M’buyuni Kata ya Ng’apa mshitakiwa akiwa anatambua kitendo anachokifanya ni kosa, alimbaka Msichana huyo  kwa udanganyifu wa kumpa fedha Shilingi 5,000/- na kukamatwa na Askari Mgambo wa Kata hiyo.

MWISHO.        

Post a Comment

0 Comments