SHARIFA MKWANGO MWENYEKITI MPYA TWFA MKOA WA LINDI.

SHARIFA  MKWANGO MWENYEKITI MPYA TWFA MKOA WA LINDI

NA HADIJA OMARY. 


LINDI.....Sharifa Mkwango ameshinda kuwa Mwenyekiti mpya wa chama cha mpira wa miguu Wanawake  (TWFA) Mkoa wa Lindi atakaehudumu nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitano  baada ya kushinda kwa Kura za ndio. 


Uchaguzi huo umefanyika Jana huko Manispaaa ya Lindi ambao ulihusisha pia nafasi za wajumbe wawili wa kamati tendaji ambao ni Bi. Subira  Mwangata na Beatrice Victor pamoja na nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (TWFA) Bi.Sifa Mwaya.

 

Akifungua mkutano huo  Afisa Michezo wa Manispaa  ya Lindi Jamal Lisuma  kwa niaba ya Katibu tawala wa Wilaya ya Lindi hudhaifa Rashid aliwataka  viongozi watakaochaguliwa kutatua changamoto zilizopo Katika Mkoa wa Lindi upande wa soka la Wanawake ikiwemo kuongeza vilabu vya timu za Wanawake na kuanzisha ligi ya Wanawake Ngazi za Wilaya na Mkoa. 


Amesema lengo la hayo yote ni   kutafuta vipaji vya wachezaji  hao wanawake wanaoweza kuunda timu ya Mkoa inavyoweza kushiriki ligi kuu ya Wanawake Tanzania Bara.


Kwa upande wake Bi.Rukia Mkwango Mwenyekiti mpya wa (TWFA) ameahidi kufanya uhamasishaji kwa Jamii kuona Umuhimu wa kuwekeza Katika Michezo kwa watoto wa Kike.


Katibu wa kamati ya Uchaguzi Fidea Mnunduma amewapongeza wajumbe kwa kutimiza wajibu wao na kutenda haki  kwenye uchaguzi huo  na kwamba Kura zimepigwa vizuri hakuna zilizoharibika kila Mmoja ametumia  haki yake kwa kutimiza wajibu wake. 

"Kamati ya uchaguzi inawashukuru wajumbe wote  kwa ushirikiano uliouonysha lakini Leo mmeweza kupata viongozi wapya wa TWFA kamati ipo itadumu kwa miaka mnne kama mutakuwa na tatizo lolote  kamati umefungua milango njooni mutuone". 

MWISHOO

Post a Comment

0 Comments