MNADA WA NANE WA MBAAZI BEI YA JUU 1,710 NA BEI YA CHINI 1,690
NA HADIJA OMARY
Chama kikuu cha ushirika RUNALI kinachohudumu katika wilaya za Ruangwa Nachingwea na Liwale kimeongoza mnada wa Nane wa zao la Mbaazi katika ofisi ya Kata ya Stesheni wilaya ya Nachingwea.
Leo Septemba 11, 2024 takribani ya kilogramu 960,121 zimeuzwa ambapo bei ya juu ikiwa ni tsh 1,710 na bei chini ni Tsh 1,690.
Licha ya wakulima kukubali kuuza zao hilo pia wameiomba serikali kupitia chama kikuu cha ushirika RUNALI kuona namna nzuri ya kufanya mbaazi kuonekana zao bora sokoni ili bei ilete tija kwa wakulima.
Aidha Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika, RUNALI Ndg. Odas Mpunga amewaomba wakulima kuendelea kukusanya mazao katika ubora wa hali ya juu na kuacha kuchanganya na makinikia( uchafu) katika mazao yao hali ambayo inaweza kupeleka kuongezeka kwa bei ya mazao sokoni.

0 Comments