BEI YA MBAAZI YAPANDA, MRAJISI ATOA MSIMAMO WA SERIKALI USAJILI WA VYAMA.

 


Bei ya mbaazi yapanda, mrajsi atoa msimamo wa serikali usajili wa vyama.

Na Ahmad Mmow, Nachingwea. 

Bei ya mbaazi imeongezeka nakufikia bei ya juu ya shilingi 790 na bei ya chini shilingi 730 kwa kila kilo moja.

Katika mnada wa nne kwa msimu wa mbaazi wa 2025 uliofanyika leo katika kijiji cha Mpiruka B, halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kwenye ofisi kuu ya chama cha msingi cha ushirika cha Ukombozi(Ukombozi AMCOS) jumla ya kilo 4,465,465 zimeuzwa kwa bei ya juu ya shilingi 790 na bei ya chini shilingi 730 kwa kila kilo moja.

Bei hiyo ni tofauti na bei za mnada wa tatu uliofanyika wilayani Liwale. Kwani bei ya juu ilikuwa shilingi 680 na bei ya chini shilingi 640 kwa kila kilo moja.

Akizungumza baada ya wakulima kukubali kuuza kwa bei hizo, mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika wa mkoa wa Lindi, Kenneth Shemdoe alisema serikali haijafunga milango ya kusajili vyama vipya vya ushirika. Ikiwamo vyama vikuu na vyama vya msingi. Hata hivyo usajili utafanywa kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya ushirika.

Amesema maombi ya kuanzishwa vyama ambayo yatakidhi vigezo yatakubaliwa. Kwani jambo kubwa ni kutimiza vigezo na sifa za kuanzisha vyama vya ushirika.

Mrajis msaidizi huyo wa mkoa wa Lindi amesema ili kuweza kuwa na vyama vyenye nguvu na tija kwa wana ushirika dhamira ya serikali ni kuunganisha vyama ambavyo uwezo wake wa uzalishaji ni mdogo kutegemea eneo vyama hivyo vilipo. Lakini kufuta vyama ambavyo vimeshindwa kujiendesha na kuwanifaisha wakulima.

Hata hivyo Shemdoe alisisitiza kwamba maeneo ambayo yatabainika yanauhitaji wa kuanzisha vyama nakwamba yanasifa zote za kuanzishwa vyama, serikali haitasita kusajili vyama vitakavyo wahudumia wakulima wa maeneo hayo.

Alitoa wito kwa viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika, hasa AMCOS  wasimamie vizuri vyama hivyo ili viweze kuwa na uchumi mkubwa utakao viwezesha kutoa ajira kwa wananchi.

" Vyama hivi vinaweza kutoa ajira kwa   vijana wasomi na hatq madereva ambao wapo mtaani iwapo vitakuwa na miradi ya kiuchumi," alisisitiza Shemdoe.

Lakini pia kuelekea msimu wa 2024/2025 wa zao la korosho alitoa wito kwa wakulima wa zao hilo wahakikishe wadhibiti ubora kwa kupeleka sokoni  korosho zenye ubora. Akiweka wazi kwamba ubora wa zao hilo unaanzia katika hatua ya palizi hadi kuhifadhi.


Post a Comment

0 Comments