WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

 


WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

NA HADIJA OMARY 

LINDI, ....Wazee wa Nachingwea wameaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba mwaka huu. 

Wito huo  umetolewa na Afisa Uchaguzi wa Wilaya ya Nachingwea Robert Mmari alipokuwa akizungumza na wazee maarufu wa Wilaya hiyo ambapo amesisitiza   kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na msaada wa wazee utahakikisha zoezi linafanikiwa. 

Afisa Uchaguzi (W) wa Nachingwea ndugu Robert Mmari pia ameeleza kuwa sifa za mgombea na mpiga kura zimeshaainishwa Mpiga kura lazima awe na akili timamu, awe na umri wa miaka 18 au zaidi, na awe mkazi wa kitongoji husika Wananchi wote wanatakiwa kupiga kura kwenye vitongoji walivyojiandikisha, huku zoezi la kuchukua fomu za kugombea likipangwa kuanza Novemba 1. 

Aidha, ndugu Joshua Mnyang'ali, Kaimu Mkurugenzi anayemwakilisha Msimamizi wa Uchaguzi wa Nachingwea, ameonya kuwa mwananchi yeyote atakayeshindwa kujiandikisha kupiga kura kati ya Novemba 11 hadi 20, atapoteza haki ya kupiga kura Alisisitiza kuwa Halmashauri imejipanga vyema kuhakikisha wananchi wanapata elimu kuhusu uchaguzi na umuhimu wa kushiriki katika zoezi hilo. 

Kwa upande wake, Chief Nakotyo alibainisha kuwa kutakuwa na tukio maalum lenye ujumbe kuhusu maadili na hamasa ya uchaguzi litakalofanyika tarehe 7 na 8 Novemba Aliwataka wazee kuendelea kuhamasisha wananchi ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa mafanikio Vilevile, Joyce Chipanda, mkazi wa Kilimani Road, amewaasa wananchi kutopotosha wenzao na badala yake kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kulinda usalama na amani ya nchi

Mwisho

Post a Comment

0 Comments