KATIBU TAWALA WILAYA YA LIWALE AMEOMBA WANANCHI WAJITOKEZE KWA WINGI SIKU YA UZINDUZI WA JOGGING ITAKAYOFANYIKA JUMAMOSI OCTOBA 5, 2024.

 


Katibu tawala wilaya ya Liwale amewaomba wananchi rika zote kujitokeza kwa wingi siku ya uzinduzi wa jogging itakayofanyika jumamosi octoba 5,2024.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Liwale,Azilongwa Bohari, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la  Jogging inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi Jumamosi,Octoba 5 ambapo jogging hiyo ni sehemu ya kampeni ya kuhamasishaji wa  wananchi kushiriki kwa wingi kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga mara zoezi hilo litakapoanza.

Bohari amesema  jogging itasaidia kuboresha afya za wananchi watakaoshiriki pia ni fursa kwakuwa itawakutanisha wananchi wengi kwa pamoja.

Bohari amesema licha ya jogging  hiyo kuwaunganisha wananchi kupitia mazoezi lakini itakuwa sehemu ya kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kujiandikisha ili waweze kutumia haki yao ya kupiga kura kwenye uchaguzi.

Pia amesema serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha zoezi la uandikishaji linafanyika kwa ufanisi na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo ili waweze kuwa sehemu ya mabadiliko yanayohitajika kwenye jamii.

Post a Comment

0 Comments