Chinguile 'awatumia salamu mahasimu wake kiaina', ahaidi
kuwabeba madiwani na kuchangia mifuko 100 ujenzi wa jengo la mama na mtoto.
Na Ahmad Mmow, Nachingwea.
Mbunge wa jimbo la Nachingwea, Mheshimiwa Amandus Chinguile amesema hakuna diwani katika jimbo la Nachingwea atakae achwa akwame na kushindwa kumaliza safari kwa mafanikio.
Chinguile alisema hayo jana kijijini Mchonda, halmashauri ya wilaya ya Nachingwea alipozungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wa kata ya Mchonda.
Bila kufafanua ni safari gani Chinguile aliahidi kushirikiana na kusaidiana na madiwani ili kuhakikisha hakuna atakae achwa nyuma na kukwama.
Katika hali inayoonesha alikuwa hatanii, amehaidi kutoa mipira mchezo wa soka na pete kwa kila kata kwa idadi ya vijiji vilivyopo kwenye kata hizo. Huku pia akiahidi kutoa jezi.
Mbali na hayo, Chinguile pia ameahidi kuchangia mifuko 100 ya saruji itakayotumika kwa ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati ya Mchonda.
0 Comments